Umaarufu wa winga wa Yanga Bernard Morrison unazidi kupenya kila kona ya nchi ya Tanzania kutokana na umahiri wake tangu alipojiunga na mabingwa hao wa kihistoria Mwezi Januri mwaka huu
Haishangazi kuona picha hiyo juu imepata umaarufu sana kwenye mitandao ya kijamii ambapo basi la abiria huko mkoani Mtwara limebandika picha zake na kuweka ujume maalum unaotumiwa sana na Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz 'Wape Salaam'

Morrison ameeleza kufurahishwa na ujumbe huo ambapo amesema unadhihirisha kwa kiasi gani mashabiki wa Yanga wana upendo wa kipekee kwa wachezaji wao
Morrison amekiri matukio ya aina hii ndio mara ya kwanza kuyaona kwani pamoja na kucheza katika nchi nyingi, hakuwahi kupata heshima kubwa kama anayopewa hapa Tanzania
Miongoni mwa matukio ambayo amesema hawezi kuyasahau ni pamoja na lile la kuchangiwa fedha zaidi ya laki tano na mashabiki wa Yanga mkoani Singida walipokwenda kucheza na Singida United
Lakini pia wilayani Ruangwa mkoani Lindi, Morrison amesema hawezi kusahau tukio la mashabiki kumsimamisha na kumpa zawadi ya kuku kuonyesha furaha yao baada ya kumuona
Morrison amesema mashabiki wa Yanga wanaipenda sana timu yao. Aidha heshima anayopewa inamfanya atamani kuendelea kucheza Yanga kwa miaka mingi zaidi