Tuko tayari, mashabiki wasubiri burudani - Nugaz

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 May 2020
Tuko tayari, mashabiki wasubiri burudani - Nugaz

Klabu ya Yanga imewataka mashabiki wake kukaa tayari kuiunga mkono timu yao kwenye michezo iliyobaki kukamilisha msimu huku wakiahidi kufunga msimu kwa kishindo

Ni baada ya kauli aliyoitoa jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk John Magufuli kuwa wiki hii anaweza kuruhusu shughuli za michezo zikarejea baada ya kujiridhisha na kasi ndogo ya maambukizi ya ugonjwa wa corona nchini

Afisa Mhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz, amewataka mashabiki wakae tayari kwani wamepania kurejea na moto usio wa kawaida

Amesema kutokana na mazoezi ambayo wanafanya wachezaji, anamini watacheza mpira wa burudani na ufundi sambamba na kushinda michezo.

"Ninachopenda kuwaambia mashabiki wa Yanga, wakae mkao wa kupokea burudani, unajua kulikuwa hakuna mechi yeyote inayochezwa, kila mmoja ana hamu ya kuona timu yake inakuja vipi"

"Sisi Yanga tunasema tunarejea kivingine, tutacheza mchezo mzuri, tunataka kila mmoja afurahi, pia tunaingia uwanjani kupambana kutafuta pointi 30," amesema Nugaz

Nugaz ameongeza kuwa pamoja na kupigania nafasi mbili za juu, watapambana kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania maarufu Kombe la Azam.

Aidha kuhusu masuala ya usajili, Nugaz amedokeza kuwa kila kitu kinaendelea kulingana na mahitaji ya mwalimu, wakati ukifika wataweka wazi wachezaji waliowasajili lakini kwa sasa bado sio wakati wake

Yanga inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa imekusanya alama 51, alama tatu nyuma ya Azam Fc inayoshika nafasi ya pili lakini Yanga ikiwa na mchezo mmoja pungufu

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael aliwahi kukiri kuwa timu yake ina nafasi finyu ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu kutokana na idadi ya pointi walizozidiwa na watani zao Simba ambao wana alama 71 huku zikiwa zimebaki mechi 10

Hata hivyo alisema watapambana kuhakikisha wanamaliza nafasi ya pili huku akiweka nguvu zaidi kwenye michuano ya kombe la FA ambayo Yanga lazima ishinde ili kupata nafasi ya kushiriki michuano ya CAF Confederation msimu ujao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’