Taarifa iliyoripotiwa na gazeti moja la michezo huko Rwanda imebainisha kuwa klabu ya Kiyovu Sport inataka kumsajili winga wa Yanga Patrick Sibomana maarufu 'PS'
Sibomana alitua Yanga dirisha la usajili lililopita akitokea klabu ya Mukura Victory
Hata hivyo tangu kutua kwa kocha Luc Eymael, Mnyarwanda huyo amepoteza nafasi kwenye kikosi cha kwanza
Aidha tetesi zaidi zimekuwa zikimuweka miongoni mwa wachezaji wa kigeni ambao wanaweza wakaachwa huru ya Yanga mwishoni mwa msimu
Kulingana na gazeti hilo, Kiyovu Sport imempa Sibomana ofa ya mkataba wa miaka miwili
"Kila kitu kuhusu mkataba kiko sawa, kinachosubiriwa na kusaini tu," kilitaarifu chanzo cha gazeti hilo
ADVERTISE HERE