Mahadhi apewa ruksa kurejea dimbani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 May 2020
Mahadhi apewa ruksa kurejea dimbani

Daktari wa klabu ya Yanga Dk Sheky Mngazija amesema kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Juma Mahadhi amepona majeraha yaliyomuweka kwa zaidi ya miezi 20 na yuko tayari kurejea uwanjani

Mngazija amesema kwa sasa nyota huyo hana tatizo lolote, atajumuika kwenye mazoezi na wachezaji wengine tayari kwa mechi za lala salama kumaliza msimu

Aidha Mngazija amesema wachezaji wengine wote wako tayari kuendelea na majukumu yao isipokuwa mlinda lango Ramadhani Kabwili ambaye hivi karibuni alipata ajali ya pikipiki

"Kabwili alipata ajali, akashonwa nyuzi nane, yeye bado anaendelea na matibabu lakini wachezaji wengine wote wako tayari kurejea uwanjani," amesema

Yanga inatarajiwa kuanza maandalizi ya pamoja baada ya Serikali kuruhusu timu zianze kufanya mazoezi kabla ya msimu kurejea Juni 01 kwa ajili ya kumalizia mechi zilizobaki

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’