Ilikuwa kama ndoto, sasa ni kweli

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
30 May 2020
Ilikuwa kama ndoto, sasa ni kweli

Mashabiki wa Yanga wanahesabu masaa tu washuhudie tukio kubwa kabisa na la kihistoria kwa timu yao kuanza rasmi mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa Uendeshaji wa klabu hiyo

Furaha zaidi ni pale watakapoishuhudia kampuni ya La Liga inayosimamia ligi kuu ya Hispania ambayo ndio inayotawala soka la Ulaya, ikiingia kandarasi ya kusimamia mabadiliko ya uendeshaji Yanga

Mpaka kufikia hatua hii uongozi wa Yanga chini ya Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla wanastahili pongezi kwani huko nyuma kuna viongozi walijaribu kufanya mabadiliko bila ya mafanikio

Lakini pia huwezi kuzungumzia mabadiliko haya yanayokwenda kutimiza ndoto za Wanayanga bila ya kuitaja kampuni ya GSM

GSM wamejitoa kwa dhati kuhakikisha wanaifanya Yanga kuwa taasisi kubwa inayojitegemea sawa na jina lake

Si jambo rahisi kujitolea kugharamia mchakato wa mabilioni kama huu, GSM wanastahili kongole

Yanga ni taasisi yenye heshima kubwa na historia Tanzania na hata Afrika nzima

Kwa miaka ya karibuni ni kama heshima hiyo ilishuka kutokana na changamoto zilizoikabili timu hiyo

Lakini hakuna shaka, baada ya tukio la kusaini mkataba na La Liga siku ya Jumapili, heshima ya Yanga itarejea mahali pake kwa kasi

Kwa kufanya kazi na La Liga tu, umaarufu wa Yanga utapaa kote duniani. Mabingwa hao wa kihistoria watajitengenezea fursa kedekede

Na pale mchakato mzima utakapokamilika, makampuni mengi yataigombania Yanga wakitaka kuwekeza biashara zao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
11h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’