Mohammed Rashidi kwenye rada za Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Nov 2017
Mohammed Rashidi kwenye rada za Yanga
Wakati dirisha dogo la usajili likitarajiwa kufunguliwa Jumatano ijayo, Novemba 15, tayari vigogo wa soka nchini wameanza kupigana vikumbo kusaka wachezaji wakali kuimarisha vikosi vyao.

Mshambuliaji wa Prisons Mohammed Rashidi tayari ameingia kwenye Radar za Yanga huku pia Azam FC nayo ikidaiwa kumnyemelea mshambuliaji huyo chipukizi mwenye umri wa miaka 22.

Rashidi ameuanza msimu huu kwa kishindo. Mpaka sasa tayari ameifungia Tanzania Prisons mabao sita akishika nafasi ya pili katika orodha ya vinara wa upachika mabao ligi kuu ya Vodacom.

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga zinabainisha kuwa inahitaji kusajili washambuliaji wawili katika jitihada za kuimarisha kikosi chake kilichoanza kwa kusuasua kwenye upachikaji mabao.

Washambuliaji pekee wanaotegemewa kwa sasa ni Obrey Chirwa na Ibrahim Ajib huku Donald Ngoma na Amissi Tambwe wakiwa majeruhi.

Ngoma hayupo kabisa nchini na ameingia katika mgogoro na viongozi wa Yanga baada ya kuondoka nchini bila ya ruhusa.

Tambwe hajacheza mchezo wowote msimu huu kutokana na majeruhi ya goti.

Yanga inakusudia kusajili mshambuliaji mmoja mzawa na mwingine wa Kimataifa kukiwa na uwezekano wa kuvunja mkataba wa mmoja wa washambulia hao.

Wasifu wa Mohammed Rashidi

Jina lake ni Mohamed Rashid Issa, kwa sasa anaitumika timu ya Magereza ya Tanzania Prisons iliyopo jijini Mbeya lakini malengo yake kama anavyosema ni kutaka kusakata soka nje ya Tanzania na kuwa tunu kwa Taifa katika siku za usoni.

Mohamed Rashid, ni mzaliwa wa Tabora kwa baba Mzee Rashidi Issa na Mama Fatuma Athuman akiwa ni mtoto wa tatu katika familia hiyo, na alianza kusaka kabumbu katika klabu ya Makongo United, kabla ya kujiunga na timu ya vijana ya Tanzania Prisons, Small Prisons.

Nyota yake ilianza kuoneka hapo ambapo baadae timu ya jeshi la kujenga Uchumi JKU ya Zanzibar ilimuona na kuhitaji huduma yake, alicheza hapo kwa mafanikio madogo ndipo alipojiunga na African Sports mwaka 2015 kabla ya kujiunga na Tanzania Prisons anayoitumika hadi hivi sasa.

Mpaka sasa Mohamed Rashid amefunga mabao 6 ya ligi kuu soka Tanzania bara akiwa nafasi ya pili nyuma na Mganda Emmanuel Okwi mwenye mabao 8, lakini bado hajaitwa kuitumikia timu ya taifa ya Tanzania, anasema muda wake bado haujafika, na atapoitwa basi atajitahidi kadri awezavyo ili kuweza kuisaidia timu ya Taifa kupata mafanikio.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’