Kocha Msaidizi wa Yanga Charles Mkwasa amethibitisha kuwa baadhi ya nyota wa timu hiyo wamepata majeraha katika mazoezi ya kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria
Akizungumza na redio Wasafi mapema leo, Mkwasa alisema winga Bernard Morisson, nahodha Papy Tshishimbi na beki kisiki Lamine Moro wamepata majeraha madogo
"Ni kweli baadhi ya wachezaji wamepata majeraha, Morrison, Tshishimbi na Moro. Hata hivyo sio majeraha makubwa sana tunatarajia watakuwa sawa kabla ya mchezo wetu wa kwanza, " amesema
Aidha Mkwasa amesema kwa program za mazoezi wanayoendelea nayo, timu itakuwa tayari Juni 13 kuikabili Mwadui Fc
ADVERTISE HERE