Licha ya taarifa ya awali iliyokuwa imetolewa na Daktari wa Yanga Dk Edward Bavu kuwa nahodha msaidizi Thabani Kamusoko na mshambuliaji Amissi Tambwe wamepona majeraha yao na wangeanza mazoezi Novemba 09, wachezaji hao wameshindwa kurejea dimbani.
Taarifa ya hivi karibuni iliyotolewa na Afisa habari wa Yanga Dismas Ten baada ya wachezaji hao kutoonekana mazoezini, imeeleza kuwa walirejea Hospitalini kufanya vipimo vya mwisho hivyo kinachosubiriwa ni matokeo ya vipimo hivyo.
Huenda Yanga ikalazimika kuchukua maamuzi magumu juu ya hatma ya wachezaji hao kama vipimo hivyo havitakuwa vizuri.
Tayari Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwassa amesema hawataendelea kuvumilia wachezaji majeruhi wa muda mrefu.
Donald Ngoma ni mchezaji mwingine majeruhi ambaye ameingia kwenye mgogoro na viongozi wa Yanga baada ya kuondoka 'kimyakimya' kambini kurejea kwao Zimbabwe kushughulikia matatizo yake binafsi

ADVERTISE HERE