Kikosi cha Yanga leo kinashuka kwenye uwanja wa Uhuru kumenyana na KMC ukiwa ni mchezo wa kirafiki, sehemu ya maandalizi kuelekea mechi za kukamilisha msimu
Mchezo huo utapigwa saa kumi jioni ambapo viingilio ni Tsh 5,000/- VIP na Tsh 3,000/- mzunguuko
Tangu kurejea mazoezini wiki iliyopita, Yanga tayari imecheza mechi nyingine mbili za kujipima, ikifanikiwa kushinda zote
Ilianza kwa kuichapa Transit Camp mabao 3-1 na jana asubuhi wakacheza na Dar City na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0
Kocha Msaidizi wa Yanga Charles Mkwasa amesema mchezo huo ni muhimu kwa kikosi chake kwani utamsaidia katika maandalizi ya mwisho kabla ya safari ya Shinyanga kuifuata Mwadui Fc tayari kwa mchezo wa ligi kuu Juni 13
ADVERTISE HERE