La Liga wafurahia ushirikiano na Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Jun 2020
La Liga wafurahia ushirikiano na Yanga

Rais wa La Liga Javier Tebas amesema ushirikiano wa kampuni yake na klabu ya Yanga, ni fursa itakayokuwa na manufaa kwa Yanga pamoja na La Liga

Wiki iliyopita Yanga ilifungua ukurasa mpya wa mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo ambao awamu ya kwanza unasimamiwa na La Liga wenye jukumu la kutoa mapendekezo na ushauri kwa mabingwa hao wa kihistoria

Tebas amesema mkataba walioingia na Yanga umepanua wigo wa majukumu yao ambapo watakuwa na nafasi ya kuonyesha uwezo wao katika kubadili na kuleta changamoto mpya ya maendeleo kwenye soka barani Afrika

"Kupiga chapuo uendeshaji wa kiweledi kwa soka la Afrika na Duniani kote ni dhima tulizonazo kama La Liga katika mkakati wa kujitanua kimataifa. Mkataba huu tuliosaini na GSM na Yanga ni mwanzo mzuri kwetu"

"Tunajivunia kufanya kazi na klabu ya Yanga, tunawahakikishia, huduma ya ushauri tunayokwenda kuwapatia, itakuwa na mafanikio makubwa kwa klabu hiyo," ilieleza sehemu ya taarifa iliyotolewa na Tebas kwa Wanahabari

GSM wadhamini/wahisani wa Yanga wanasimamia gharama za mchakato wote ambao mpaka kumalizika kwake utachukua miaka miwili na nusu mpaka mitatu

Katika miezi sita ya kwanza, Wataalamu wa La Liga watakuwepo hapa nchini kufanya kazi bega kwa bega na kamati ya Mabadiliko ya klabu ya Yanga inayoongozwa Wakili Msomi Alex Mgongolwa

La Liga watakuwa na jukumu la kutoa maoni na mapendekezo ya aina ya mfumo ambao Yanga wanapaswa kufuata kufuatana na mazingira yetu

Mapendekezo hayo yatajadiliwa kisha kufikishwa mbele ya Wanachama wa Yanga kupitia Mkutano Mkuu wa klabu ambao utafanya maamuzi ya Mwisho

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
8h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
11h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
16h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
20h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’