Morrison amkera Eymael

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Jun 2020
Morrison amkera Eymael

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael ameeleza kutofurahishwa na kitendo kilichofanywa na winga wa timu hiyo Bernard Morrison ambaye leo hakuuunga nae katika safari ya mkoani Shinyanga

Morrison hakusafiri na wachezaji wengine juzi baada ya kuchelewa basi, hata hivyo alimuahidi Eymael kuwa wangesafiri pamoja leo sambamba na David Molinga

Hata hivyo Eymael amesema hakuweza kumpata Morrison katika simu yake ulipofika muda wa kuondoka jijini Dar es salaam

"Sifahamu alipatwa na tatizo gani, kama kocha wake alipaswa kunieleza. Tulizungumza na kuelewana kuhusu safari hii, lakini muda ulipofika sikumuona," alisema Eymael

"Mimi sina tatizo, nitafanya kazi na wachezaji waliopo lakini kwa mchezaji wa kulipwa unapaswa kuwa makini na kazi yako, kwani unaweza kupoteza dira"

Naye Meneja wa Yanga Abeid Mziba amesema katika Hotel waliyofikia mkoani Shinyanga walifanya 'booking' ya chumba kwa ajili ya Morrison

"Sisi hatufahamu ana tatizo gani, kwani hata chumba chake tumemuandalia huku, nadhani waulizwe viongozi wanaweza kuwa na majibu," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’