Kiungo mshambuliaji wa Yanga Bernard Morrison ambaye kwa sasa ni habari ya mjini, atakuwepo mkoani Dodoma siku ya Jumatano kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania
Morrison alikosa mchezo wa jana dhidi ya Mwadui Fc huku kukosekana kwake kukiacha sintofahamu miongoni mwa mashabiki wa Yanga
Hata hivyo Mghana huyo amesema alipata maumivu ya mguu kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Dar City
Amesema yuko vizuri na Wanayanga wasubiri kumuona mkoani Dodoma akiendelea na majukumu yake katika kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria
ADVERTISE HERE