Eymael ambana Morrison, ampa masharti

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Jun 2020
Eymael ambana Morrison, ampa masharti

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amempa masharti winga Mghana Bernard Morrison kabla ya kumruhusu kurejea kikosini

Morrison hakusafiri na timu mkoani Shinyanga na hata Eymael alipomuagiza waungane nae kwenye safari yake akaingia mitini

Eymael amesema amezungumza na Morrison, ambapo ametambua makosa yake na kumuomba radhi

Hata hivyo amemwambia abaki jijini Dar es salaam asubiri timu itakaporejea na atatakiwa kuwaomba radhi viongozi, wadhamini, wachezaji, benchi la ufundi na mashabiki wa klabu ya Yanga ambao wengi hawakufurahishwa na tukio la kukosekana kwake kikosini

"Nimezungumza na Morrison kwa muda mrefu, ametambua makosa yake na nimemwambia atusubiri tukirudi Dar atatakiwa kuwaomba radhi wachezaji wenzake, viongozi, wadhamini wetu, benchi la ufundi pamoja na mashabiki wa Yanga"

"Nimempa masharti ni lazima aombe radhi au la hatutamjumuisha kwenye timu yetu itakayoanza maandalizi ya mchezo dhidi ya Azam baada ya kurejea Dar es salaam," alisema Eymael

"Natambua Morrison ni mchezaji nyota ndani ya kikosi cha Yanga lakini ni lazima atambue kung'ara kwake kunachangiwa na usaidizi wa wachezaji wenzake. Hakuna timu ya mchezaji mmoja. Hata leo ukiwachukua kina Messi wawili, Ronaldo wawili ukawaongezea na Sergio Ramos wawili, peke yao wakicheza na timu ya wachezaji 11 ni lazima watafungwa"

Morrison amekubali kuwaomba radhi wanafamilia wa Yanga huku akiwashushia lawama baadhi ya Mawakala ambao wameweka tamaa mbele kwa kumpotezea malengo yake

Juzi Morrison alifichua sakata lake na klabu ya Simba ambapo alieleza jinsi Wakala aliyetumwa na klabu hiyo anavyomhadaa ili asaini mkataba katika timu hiyo

Jana Mkurugenzi wa uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said alisema wachezaji wanapaswa kuzingatia nidhamu na hakuna mchezaji mkubwa kuliko Yanga

Wakati Yanga ikiwa Shinyanga, mshambuliaji David Molinga ambaye awali aligomea safari, alizuiwa kujumuika na wachezaji wengine mpaka pale alipowaomba radhi wachezaji wenzake na benchi la ufundi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22m ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
14h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
23h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’