Wanachama Milioni moja wanatosha kuiendesha timu - Hersi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Jun 2020
Wanachama Milioni moja wanatosha kuiendesha timu - Hersi

Mapema leo, Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said alishiriki hafla ya uzinduzi wa Tawi la klabu ya Yanga Makao Makuu mkoani Dodoma

Akizungumza katika hafla hiyo, Hersi amesema Yanga inahitaji kusajili angalau Wanachama Milioni moja tu ambao watakuwa na uhakika wa kulipa ada ya kila mwaka ambayo ni Tsh 12,000/- (Tsh 1,000/- kwa mwezi)

"Kama wanachama milioni moja (1,000,000) watalipa ada ya uanachama klabu itaweza kupata Tsh. 12 bilioni kwa mwaka," alisema

"Gharama za kuiendesha klabu hazizidi Tsh. 4 bilioni kwa mwaka. Tutaweza kusajili wachezaji wenye hadhi na kulipa mishahara tarehe 20 ya kila mwezi, tutakuwa na uwezo wa kujenga uwanja wa mazoezi na kuboresha jengo la klabu na kuwa la kisasa"

"Tukiweza kuwa na Tsh. 12 bilioni kwa mwaka hatuhitaji mtu mmoja kwa ajili ya kuendesha klabu yetu, hatutaki mtu mmoja akinuna basi wanayanga wote tunanuna," alisema Hersi

Β Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, Yanga ina mashabiki zaidi ya Milioni 15, kinachotakiwa kufanyika ni kuwabadili mashabiki hao kuwa Wanachama ambao watachangia maendeleo ya klabu yao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’