Viwanja vya mikoani vyamchefua Eymael

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Jun 2020
Viwanja vya mikoani vyamchefua Eymael

Kocha wa Yanga, Luc Eymael, amesema soka la Tanzania haliwezi kufanikiwa kama wachezaji wataendelea kucheza kwenye viwanja vibovu.

Eymael ametoa kauli hiyo kutokana na ubovu wa baadhi ya viwanja vinavyotumika kwenye ligi hiyo.

Juzi Yanga ilibanwa na kutoka sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma, ambao kocha huyo ameulalamikia kwa ubovu.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Eymael alisema ubovu wa sehemu ya kuchezea kwenye uwanja huo ilichangia kikosi chake kukosa ushindi ambao walikuwa wamedhamiria kuupata, ikiwa ni maandalizi ya mchezo dhidi ya Azam FC unaotarajiwa kuchezwa Jumapili ijayo.

"Soka la Tanzania haliwezi kufanikiwa na wachezaji kucheza vizuri na kupata matokeo mazuri kama wataendelea kucheza kwenye viwanja ambavyo siyo rafiki, mpira hautulii muda wote unarukaruka na pasi zikitolewa zinashindwa kufika kwa mlengwa," alisema Eymael.

Alisema hata kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mwadui FC, walioshinda bao 1-0, uwanja walioutumia ulikuwa na shida hiyo hiyo na wachezaji wake walishindwa kujituma kwa kuhofia usalama wa afya zao kwa kuwa wanategemea mpira kama kazi ya kuendesha maisha yao.

Pia Eymael amemuombea msamaha kwa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Lamine Moro, aliyeoneshwa kadi nyekundu kwenye mechi hiyo kwa kumchezea vibaya, Mwinyi Kazimoto.

"Hali hiyo imemkuta akiwa kwenye kazi, hivyo TFF wamsamehe kwani mchezaji huyo kakosea kama binadamu mwingine, hivyo waangalie, nadhani atajirekebisha kwani hata mwenyewe anajutia tukio alilolifanya," alisema Eymael

Kwa upande wake Moro ameeleza kujutia kitendo hicho na kuomba msamaha kwa Kazimoto, wapenzi na wadau wa mchezo huo na kuahidi kutorudia tena.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’