Uongozi wa klabu ya Yanga umewataka mashabiki kuiunga mkono timu yao kuelekea mchezo dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa baadae leo kwenye uwanja wa Taifa
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema kikosi chao kiko imara, hawatakisiki na wamepania kuondoka na alama zote tatu saa moja jioni ya leo
Yanga itashuka katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kulazimishwa sare katika michezo yake miwili iliyopita
Ni mchezo muhimu ambao matokeo ya ushindi yanaweza kurejesha furaha ya mashabiki ambao kwa siku za karibuni timu yao imekumbana na changamoto za nje ya uwanjani
ADVERTISE HERE