Mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga, Bernard Morrison anadaiwa kuondoka nchini na kuelekea Afrika Kusini bila ya kupata ruhusa kutoka kwa uongozi wa klabu yake, imefahamika
Taarifa zilizopatika jijini Dar es Salaam jana zinasema Morrison alitoroka katika kambi ya timu hiyo tangu juzi usiku, wakati akiwa ni sehemu ya mipango ya kikosi cha kilichoivaa Kagera Sugar jana usiku.
Chanzo chetu kiliendelea kusema nyota huyo alitofautiana na viongozi wa timu waliokuwapo kambini baada ya kukataliwa kuondoka.
"Ni kweli hayupo kazini, alitoroka kambini, ameondoka kwa mabavu, kuna mambo mengi yanaendelea kumhusu mchezaji huyo," kiliongeza chanzo chetu
Nyota huyo ambaye alifunga bao pekee katika mchezo wa watani wa jadi Machi 8, mwaka huu, aliendelea kutokuwa na mahusiano mazuri na viongozi wake baada ya kutakaa kuvunja mkataba mpya wa miaka miwili ambao alisaini hivi karibuni