Yanga imepania kwelikweli kupata matokeo mazuri katika mechi zote zilizobaki ligi kuu ya Vodacom ili kuhakikisha wanamaliza kwenye nafasi ya pili
Lakini lengo kuu ni kushinda taji la FA ili kujipatia tiketi ya kushiriki michuano ya CAF msimu ujao
Kazi inaanza Musoma leo, halafu wapambanaji wanaelekea Kagera kuchukua alama nyingine tatu kabla ya kupeleka kilio pale mitaa ya Msimbazi Julai 12
Wachezaji wa Yanga wanafahamu umuhimu wa mechi hizi za mwishoni mwishoni hasa ikizingatiwa kuna mchakato mkubwa wa kukisuka upya kikosi kwa ajili ya msimu ujao
Kwa wachezaji watakofanya vizuri, watakuwa na nafasi ya kuendelea kubaki na mabingwa hao wa kihistoria
Hivi karibuni kocha Eymael alifichua kuwa atampa kila mchezaji nafasi kwenye mechi hizi za lala salama ili awe na maamuzi sahihi kwenye usajili