Eymael aweka mkakati wa ushindi Jumapili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Jul 2020
Eymael aweka mkakati wa ushindi Jumapili

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema mchezo wa nusu fainali ya kombe la FA dhidi ya Simba ambao utapigwa keshokutwa Jumapili, ni wa kufa au kupona

Baada ya kukosa ubingwa wa ligi kuu, Eymael amesema ubingwa wa kombe la FA ndio utawapatia nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao, hivyo hawana namna zaidi ya kushinda mchezo huo

Mbelgiji huyo amesema wanafahamu mchezo hautakuwa mwepesi kwa sababu unahusisha vilabu vyenye upinzani wa jadi, lakini pia matokeo ya ushindi ambao Yanga waliyapa kwenye mchezo uliopita baina yao, unawafanya Simba wakamie mchezo huo wakitaka kulipa kisasi

"Hii mechi itakuwa ngumu sana, kwa sababu Simba wanataka kulipa kisasi kwani tuliwafunga mchezo uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini wote tunataka kuingia fainali na kutwaa ubingwa huu,” alisema.

"Sisi mchezo huu una umuhimu mkubwa sana kwetu, kwani inaweza ikawa njia ya kushiriki michuano ya kimataifa, na tumejiandaa tunamaliza kazi mapema," alisema Eymael

Baada ya ushindi dhidi ya Kagera Sugar kule Bukoba, Yanga iliendelea kubaki mkoani humo ikijiandaa na mchezo huo, kikosi kikitarajiw akurejea jijini Dar es salaam leo kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya mwisho

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
15h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
19h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
22h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’