Hatutakubali kumaliza msimu bila kombe - Eng Hersi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Jul 2020
Hatutakubali kumaliza msimu bila kombe - Eng Hersi

Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amesema maandalizi ya mchezo dhidi ya Simba yamekamilika na wana kila sababu ya kushinda mchezo huo ili kutinga fainali

Hersi yuko na kikosi cha Yanga huko Bukoba akisimamia masuala muhimu kuelekea mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini

Amesema kombe la FA  ndio nafasi pekee kwao kuweza kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao. Lakini pia, amesema GSM kama moja ya wadhamini hawako tayari kuona Yanga inakwenda msimu wa tatu bila kushinda taji lolote

"Ni aibu kwa timu kubwa kama Yanga katika ukanda huu wa Afrika kushindwa kuchukua kombe, hivyo kama wadhamini tumepanga kufuta aibu hiyo kwa kuhakikisha tunafanya kila liwezekano lililokuwepo ndani ya uwezo wetu ili tuchukue ubingwa huu"

"Tumeandaa kambi nzuri na bonasi za wachezaji kuelekea mchezo ujao wa nusu fainali dhidi ya Simba, lengo ni kuwaongezea morali wachezaji ya kupambana ili malengo yetu ya kuchukua kombe hilo yatimie"

Kama ilivyokuwa mchezo wa March 08, wachezaji wa Yanga 'watasepa' na Mamilioni kama wataifunga Simba na kutinga fainali ya michuano ya kombe la FA ambayo bingwa wake atakwenda kupatikana mkoani Rukwa

Katika mchezo uliopita dhidi ya Simba, GSM walitoa bonus ya Tsh Milioni 200, inaelezwa fedha walizoahidiwa wachezaji kama watashinda Jumapili  ni zaidi ya kitita hicho

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
21h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
22h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’