Nani aanze, nani asubiri?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Jul 2020
Nani aanze, nani asubiri?

Siku ya kesho Jumapili, kikosi cha Yanga kitashuka katika uwanja wa Taifa kumenyana na watani zao Simba katika mchezo muhimu wa nusu fainali michuano ya kombe la FA (ASFC)

Yanga inasaka nafasi ya kutinga fainali ya michuano hiyo ambayo itapigwa kule mkoani Rukwa, katika uwanja wa Nelson Mandela

Kocha Luc Eymael atakuwa na kazi ya kuchagua wanaume 11 ambao watapewa jukumu la kuhakikisha wanaipeleka Yanga fainali

Ukimuondoka Mapinduzi Balama, nyota wengine wa kikosi cha kwanza wako tayari kwa mchezo huo

Siku mbili nyuma kulikuwa na wasiwasi juu ya hatma ya kiungo Haruna Niyonzima na nahodha Msaidizi Juma Abdul ambao walipata majeraha kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Biashara United

Jana Eymael alibainisha kuwa wachezaji hao walifanya mazoezi na wenzao vizuri hivyo wana zaidi ya asilimia 50 kushiriki mchezo huo

Bila shaka, langoni Eymael ataendelea kumuamini Metacha Mnata licha ya Farouk Shikhalo kufanya vizuri katika michezo ya karibuni

Abdul anaweza kurejea upande wa kulia kama madaktari watajiridhisha na hali yake lakini hata akikosekana nafasi hiyo anaweza kuwekwa Deus Kaseke ambaye ameonyesha kuimudu vyema

Jaffar Mohammed ndiye anayeangaliwa zaidi upande wa ulinzi wa kushoto wakati pale kati wababe Lamine Moro na Said Juma Makapu watasimama wawili kuwadhibiti washambuliaji wa Simba

Kama Tshishimbi hatakuwa vizuri, nafasi ya kiungo mkabaji huenda akakaa mkongwe Kelvin Yondani au Abdulaziz Makame 'Bui' kutegemeana na mbinu ambayo Eymael ataingia nayo

Hakuna shaka Kaseke anastahili kuwa na nafasi kwenye kikosi kitakachoanza hapo kesho, winga ya kulia anaweza kuonekana wakati mwenye mkuki wa sumu, Bernard Morrison atatokea winga ya kushoto

Huu unaweza kuwa mchezo wa kwanza wa dabi kwa mshambuiliaji David Molinga 'Falcao' kama Eymael ataamua kuanza nae.

Lakini pia kasi na nguvu za Ditram Nchimbi zinaweza kuhitajika kuwapa wakati mgumu walinzi wa Simba ili kumrahisishia kazi Morrison

Fundi Niyonzima anaweza kuwepo pale kati akishirikiana na Feisal Salum 'Fei Toto' kuhakikisha ushindi unapatikana. Lakini nje atakuwepo Mohammed Issa 'Banka' ambaye alijumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 26 walioingia kambini kujiwinda na mchezo huo

Hii ni mechi ya kufa au kupona kwa Yanga, hakuna matokeo mengine zaidi ya ushindi. Kwani hatma ya ushiriki wa michuano ya Kimataifa msimu ujao, imeshikiliwa na mchezo huu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
14h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
18h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
19h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
19h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’