Nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi leo ameshiriki kikamilifu mazoezi ya mwisho ya mabingwa hao wa kihistoria kuelekea mchezo wa nusu fainali kombe la FA dhidi ya Simba ambao utapigwa kesho Jumapili Julai 12 kwenye uwanja wa Taifa
Tshishimbi hakujumuishwa kwenye kikosi cha Yanga kilichokuwa kanda ya ziwa kutokana na majeraha
Mcongomani huyo ameshiriki mazoezi hayo ya mwisho akionekana kuwa fiti kuwavaa Simba hapo kesho
Katika moja ya mahojiano yake hivi karibuni, Tshishimbi alisema atawashawishi mabosi ya benchi la ufundi la Yanga wampe nafasi ya kucheza siku ya Jumapili hata kwa kipindi kimoja
Kuna kila dalili atashuka dimbani Jumapili..!




ADVERTISE HERE