Ngasa, Kabamba, Boxer wawashangaza mashabiki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Jul 2020
Ngasa, Kabamba, Boxer wawashangaza mashabiki

Mawinga Mrisho Ngasa na Erick wamekuwa wakifanya vizuri katika mechi wanazopewa nafasi ya kucheza lakini inashangaza hawana nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza

Jana Ngasa alikuwa chachu ya ushindi dhidi ya Singida United, akitoa pasi moja ya bao huku akifunga bao pia

Ngasa amekuwa na mwendelezo mzuri kila anapopewa nafasi, lakini ni kama haaminiwi na kocha Luc Eymael

Mzambia Kabamba alisajiliwa na Yanga mwezi Januari usajili wa dirisha dogo, lakini kama kumbukumbu ziko sawa, hakucheza zaidi ya michezo mitano

Cha kushangaza, Kabamba amekuwa akionyesha uwezo mzuri katika mechi anazopewa nafasi

Ni wazi kama angecheza mara kwa mara pengine angeweza kuwa msaada mkubwa kwa Yanga kuliko hata kina Bernard Morrison ambao waliaminiwa kiasi kujiona ni wakubwa kuliko Yanga

Mchezaji mwingine aliyekalia sana 'ubao', ni beki Paulo Godfrey 'Boxer' ambaye msimu uliopita alikuwa miongoni mwa wachezaji bora wa Yanga

Tangu kuondoka kwa Mwinyi Zahera, Boxer alishindwa kupenya kwenye kikosi cha Eymael hata baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje kwa zaidi ya wiki 12

Pengine ni wakati kwa benchi la ufundi kuwatumia wachezaji hao mara kwa mara katika mechi zilizobaki kwani wanaweza hata kustahili kuwemo kwenye kikosi cha Yanga cha msimu ujao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
10h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
14h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
19h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
22h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’