Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema tetesi za kuwa wako mbioni kumsaji beki wa kushoto wa Simba Gadiel Michael hazina ukweli wowote
Eymael amesema sio Gadiel tu, bali hawana mpango wa kumsajili mchezaji yeyote kutoka klabu ya Simba
"Hapana ,tulishasajili mlinzi wa kushoto ambaye anatoka nje nchi pia hatujawahi kumtaka mchezaji yoyote kutoka ndani ya kikosi cha Simba," amesema Eymael
Tangu jana tetesi zinazomuhusisha Gadiel kutaka kurejea Yanga zimeripotiwa sana kwenye mitandao ya kijamii
Gadiel aliondoka Yanga katika mazingira ambayo hayakuwafurahisha mabosi wa timu hiyo akienda kujiunga na Simba
Alipewa mkataba kabla ya kwenda kushiriki michuano ya Afcon na kikosi cha Stars nchini Misri hata hivyo hakuusaini mkataba huo na akasubiri siku mbili kabla ya dirisha la usajili kufungwa akatangaza kujiunga na Simba
Mashabiki wa Yanga wameonekana kuchukizwa na tetesi za mchezaji huyo kuhusishwa na mabingwa hao wa kihistoria kutokana na matukio aliyofanya msimu uliopita