Mkwasa, Manyika wana udhuru - Bumbuli

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Jul 2020
Mkwasa, Manyika wana udhuru - Bumbuli

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amefafanua kuwa kocha Msaidizi wa timu hiyo Charles Mkwasa pamoja na kocha wa makipa Peter Manyika wameshindwa kusafiri na timu mkoani Morogoro kutokana na udhuru na hakuna mgogoro baina yao na kocha mkuu Luc Eymael

Bumbuli aliyeongozana na timu mkoani Morogoro, amesema taarifa nyingi zinazoripotiwa zikidai kuwepo mgogoro baina ya makocha hao hazina ukweli wowote

"Hakuna mgogoro wowote kwenye benchi letu la ufundi kama inavyokuzwa na vyombo vya habari. Kocha wetu Msaidizi (Mkwasa) aliomba asijumuishwe katika safari ya mkoani Morogoro na Iringa kutokana na Afya yake, baada ya kusafiri sana aliomba apumzike apate wasaa wa kufanya vipimo," alisema Bumbuli

"Manyika yeye alipata msiba wa kufiwa na mtoto wa Dada yake hivyo nae aliomba asisafiri na timu. Wote wawili walimpa taarifa kocha (Eymael) ingawa awali hakukubaliana nao kirahisi, lakini mwisho wa siku aliridhia"

“Kwa ujumla hakuna tatizo kubwa ila sema baadhi ya watu wasioitakia mema klabu yetu wanataka kuivuruga. Manyika yeye ataungana na timu baada ya mechi dhidi ya Mtibwa tayari kwa safari ya kwenda kuivaa Lipuli mjini Iringa,”aliongeza Bumbuli

Baadae leo Yanga itashuka kwenye uwanja wa Jamhuri kumenyana na Mtibwa Sugar kisha kuelekea Iringa kukamilisha msimu kwa kuikabili Lipuli Fc

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’