Vipi babu arudi?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Jul 2020
Vipi babu arudi?

Tetesi zimekuwa nyingi sana wakati siku moja tu ikiwa imesalia kabla ya msimu wa ligi kuu ya Vodacom kufika tamati na timu kuanza maandalizi ya msimu ujao

Hans van Pluijm ndio kocha wa mwisho kuipa Yanga ubingwa wa ligi kuu, msimu wake wa mwisho nusu ya kazi yake ilimaliziwa na George Lwandamina, raia wa Zambia

Ndiye aliyeunda kikosi kilichotwaa ubingwa wa ligi kuu kwa misimu mitatu mfululizo

Katika misimu miwili na nusu aliyokuwa na mabingwa hao wa kihistoria, alijizolea sifa kwa kuunda timu iliyokuwa ikitandaza soka maridadi

Wakati wake aliwasajili nyota wengi waliotamba Yanga wakiongozwa na Donald Ngoma, Thabani Kamusoko na Obrey Chirwa lakini pia alikuwa chachu ya kuwaibua akina Yusufu Mhilu, Juma Mahadhi bila kumsahau Simon Msuva ambaye aliweza kumfanya awe mchezaji wa kutegemewa kwenye kikosi cha kwanza

Za chinichini ni kwamba huenda 'Babu' Pluijm anaweza kurejea Jangwani, mabosi wa Yanga wakifikiria mpango wa kuvunja benchi lote la ufundi

Mbelgiji Luc Eymael anaweza kuponzwa na mwenendo wa kusuasua wa kikosi chake akiweka rekodi ya kupata sare 15 licha ya kuwa suala la uimara wa kikosi linaweza kuwa limechangia

Je Pluijm anaweza kuirejesha Yanga katika zama zile za kampa-kamtena, kapigwa-kapigwa tena...?

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’