Aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema hawezi kutekeleza ahadi ya kukatwa mkono au kutoa dola 1,000 aliyoiweka endapo Molinga hata fikisha magoli 15 kwenye ligi msimu huu
Zahera amesema Molinga alikuwa hapangwi makusudi kwenye baadhi ya mechi ili asifikishe idadi ya magoli ambayo yeye alisema atafikisha
"Nimefurahi sana kwa sababu ni mchezaji ambaye mimi ndio nilimleta, nasikitika kidogo kwa sababu hakucheza mechi 10, alicheza mechi 28 na kufunga magoli 11. Kama angecheza hizo mechi 10 angefikisha magoli 15 au zaidi"
"Siwezi kutekeleza ahadi kwa sababu kuna watu walikuja katikati na kuweka ukuta ili Molinga asifikishe magoli 15. Wewe umeona wapi mchezaji anayeongoza kwa magoli kwenye klabu yake anaachwa nyumbani au anawekwa benchi bila sababu?"
"Kama angecheza mechi zote halafu asifikishe idadi ya magoli niliyotaja basi ningetekeleza ahadi niliyoitoa,"Β alisema Zahera
Molinga amemaliza msimu akiwa amefunga magoli 11 na assist 1, huku akifunga mabao mawili kwenye michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)