Simba imejiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Vodacom baada ya kuilaza Prisons bao 1-0 katika moja ya michezo ya VPL iliyopigwa leo.
Nayo Ruvu Shooting imepata ushindi wake wa kwanza msimu huu baada ya kuilaza Ndanda FC bao 1-0.
Majimaji imeitungua Mbao FC mabao 2-1 wakati Stand United imetoshana nguvu na Mwadui FC baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana.
Simba inaendelea kukaa kileleni ikiwa na alama 22 baada ya kushuka dimbani mara 10. Azam FC, na Yanga zote zitashuka dimbani kesho Jumapili kukamilisha mzunguuko wa 10.
Yanga itakuwa kwenye uwanja wa Uhuru ikiikarinisha Mbeya City katika mchezo ambao ni lazima ipate ushindi ili iendelee kuweka hai matumaini yake ya kutetea ubingw kwa msimu wa nne mfululizo.

ADVERTISE HERE