Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Mwanasheria Simon Patrick amesema awamu ya kwanza ya mchakato wa Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji klabu ya Yanga, itakamilika mwishoni mwa mwezi huu, August 30 2020
Simon amesema hatua itakayofuata baada ya mchakato huo kukamilika, utapelekwa kwa Wanachama kwenye Mkutano Mkuu kwa ajili ya kupitishwa
Simon amewataka Wanayanga kuwa watulivu wakati timu ikiendelea kujiweka sawa huku akibainisha kuwa wanaweza kushiriki usajili kwa kubofya *149*40# au kupitia App rasmi ya klabu ya Yanga
Hatusajili kushindana na timu moja
Katika hatua nyingine, Simon amesema usajili unaofanywa na Yanga sio kwa ajili ya kushindana na timu moja
Jana Mwanahabari Shaffih Daudi kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii alitoa maoni yaliyokosoa usajili wa Yanga kuwa hawataweza kushinda ubingwa mbele ya Simba
"Hatufanyi usajili kushindana na timu moja, 'Underdogs will always reason like underdogs' "