FT : Yanga 5-0 Mbeya City

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Nov 2017
FT : Yanga 5-0 Mbeya City
Katika siku ambazo Mbeya City haitasahau ni leo ilipokumbana na Yanga iliyokuwa na uchu wa kuibuka na ushindi katika dimba la Uhuru.

Mbeya City wamejikuta wakiokota mpira nyavuni mara tano baada ya kukubali kipigo cha mabao 5-0 kutoka kwa mabingwa mara tatu mfululizo ligi kuu ya Vodacom Yanga.

Yanga ilianza kuhesabu bao la kwanza kwenye dakika ya 19 kupitia kwa nyota wa mchezo huo Obrey Chirwa aliyeunganisha krosi ya Pius Buswita aliyemzidi ujanja mlinzi wa Mbeya City aliyekuwa akisubiri mpira utoke.

Dakika tatu baadae Emanuel Martin akaweka kambani bao la pili maridadi kabisa baada ya kupkea pasi murua kutoka kwa Raphael Daudi.



Kwenye dakika ya 27 Pius Buswita nusura aipatie Yanga bao la tatu baada ya kumpiga chenga mlinda lango wa Mbeya City, mpira wake hafifu haukuweza kutinga wavuni kabla Emanuel Martini hajaukwamisha tena lakini akawa amemfanyia madhambi mlinzi wa Mbeya City.

Yanga ikicheza kandanda safi ya kushambulia kwa kushitukiza ilipendezeshwa zaidi na Pato Ngonyani, Ibrahim Ajib na Raphael Daudi waliokuwa wakianzisha mashambulizi kwa ustadi mkubwa.

Mpaka mapumziko Yanga ilitoka kifua mbele kwa mabao 2-0.

Iliwachukua dakika tano tu Yanga kuandika bao la tatu kwenye kipindi cha pili, mfungaji akiwa Obrey Chirwa kupitia mkwaju wa penati.

Ilikuwa ni pasi murua aliyotanguliziwa Raphael Daudi ambaye alifanyiwa madhambi na mlinda lango wa Mbeya City baada ya kumramba chenga ndani ya eneo la hatari.

Chirwa akaifungia Yanga bao la nne kwenye dakika ya 59 baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa Ibrahim Ajib ambaye hakika Yanga ina kila sababu ya kujivunia kuwa nae.

Ajib alipumzishwa kwenye dakika ya 60 na mwalimu Lwandamina nafasi yake ikichukuliwa na Geofrey Mwashiuya.

Emanuel Martini aliifungia Yanga bao la tano kwenye dakika ya 80 akiunganisha krosi ya Gadiel Michael aliyewatoka walinzi wa Mbeya City kabla ya kumpasia Martini.

Kocha Lwandamina alifanya mabadiliko kwenye dakika 10 za mwisho kwa kuwaingiza Yusuph Mhilu na Juma Mahadhi nafasi za Obrey Chirwa na Pius Buswita.

Chirwa alikuwa mwiba mkali baada ya kuifungia Yanga mabao matatu 'hat-trik'.

Hiyo ni hat-trik ya pili msimu huu baada ya ile ya Emanuel Okwi dhidi ya Ruvu Shooting.

Chirwa sasa amefikisha mabao sita sawa na Mohammed Rashidi wa Prisons wakiwa na mabao mawili nyuma ya Emanuel Okwi mwenye mabao nane.

Licha ya ushindi Yanga imeendelea kubaki nafasi ya tatu ikiwa na alama 20.

Azam FC imeilaza Njombe Mji bao 1-0 hivyo kusalia nafasi ya pili baada ya kufikisha alama 22 sawa na Simba.

Mtibwa Sugar imepoteza mchezo wa kwanza msimu huu mbele ya ndugu zao Kagera Sugar kwa kulazwa bao 1-0.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’