Huko Jangwani mambo yanaendelea kunoga, ni kuelekea tukio la wiki ya Mwananchi ambapo upo uwezekano mkubwa miamba wa soka nchini Hispania na mabingwa mara tatu mfululizo ligi ya Europa, Sevilla wanaweza kuwa waalikwa kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi itakayofanyika baadae mwezi huu
Kwa wasio fahamu katika moja ya vipengele ambavyo Yanga na La Liga waliingia makubaliano, ni kuitumia klabu ya Sevilla kuwa sehemu ya kujifunza na kuwa na ushirikiano katika masuala ya uongozi na hata timu zote kuanzia ya vijana, Wanawake na kikosi cha kwanza
Sevilla wanaweza kutua nchini kunogesha kilele cha wiki ya Mwananchi ambayo kwa hakika litakuwa ni tukio la kihistoria
Uzinduzi wa wiki ya Mwananchi utafanyika mkoani Dodoma siku ya Jumamosi, August 15 2020
GSM wanatembea mulemule kwenye ahadi zao, kwa hakika wanastahili pongezi