Tulieni, mambo mazuri zaidi yanakuja

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Aug 2020
Tulieni, mambo mazuri zaidi yanakuja

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Simon Patrick amesema katika hatua ya kwanza ya mchakato wa Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji, wamedhamiria kufanya mambo makubwa matatu

Mambo hayo pia yliwahi kuzungumzwa na Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said ambayo yanajumuisha Mfumo sahihi wa uongozi, benchi bora la ufundi na wachezaji wa kiwango cha juu

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Simon ameandika haya;

Katika mabadiliko ya kweli tunayoyataka wana Yanga, kama tulivyosema hapo awali, tutaanza na mambo makuu matatu;

Proper Management: Kwenye phase ya kwanza ya mabadiliko ya kimfumo, Klabu yetu itapendekeza kwa wanachama mfumo wa kisasa wa Uongozi kwenye vilabu (Modern Organizational Structure) na kuruhusu uwekezaji huku Klabu ikibaki ni mali ya wanachama kwa asilimia zaidi ya hamsini.

Katika mfumo huu, muwekezaji atanunua hisa kwanza ndipo atapata uhalali wa kuwa mwanahisa “shareholder” na sio kwa ahadi

Proper Technical Department: Tutatengeneza bench la ufundi lililo bora kuweza kuzisaidia timu zetu nje na ndani ya uwanja kwa weredi mkubwa sana na wa kisasa

Top Class Players: Tutajenga timu yenye ushindani mkubwa sana na nidhamu ya hali ya juu, na usajili utafanywa kwa weredi mkubwa sana bila ujanja ujanja, mihemko huku tukizingatia kanuni za usajili.

Utekelezaji wa haya yote ndio kiashiria halisi cha mabadiliko “Transformation”.

Wananchi wenzangu naomba mnielewe ninavyowaambia msikubali kuyumbishwa, kuna watu hawafurahii mabadiliko haya, yanawaogopesha sana watu ndio maana wanajaribu kutuvuruga lakini hawataweza.

Klabu ya Yanga inaenda kuweka historia ya kuwa Klabu ya KWANZA kufanya real transformation Tanzania katika vile vilabu vinavyomilikiwa na wananchi, hili ni la kujivunia, na tulilinde kwa nguvu zetu zote

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’