Pamoja na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kuwa tayari kupitia upya hukumu ya sakata la Morrison, lakini nadhani ni vyema Yanga ikaenda Mamlaka za juu zaidi kwani kesi hiyo hata ikisikilizwa mwaka mzima na Kamati hiyo, haiwezi kutoa majibu tofauti
Mpaka sasa inaelezwa bado nakala ya hukumu haijatolewa licha ya uongozi wa Yanga kuiomba wapatiwe ili waweze kwenda kufungua shauri kule kwenye Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa michezo (CAS)
Wadau wameonyesha wasiwasi kuwa hukumu inaweza ikachukua muda mrefu kutolewa kwa kuwa maamuzi ya Kamati yalikuwa na utata mwingi
Shauri hili linatakiwa lifikishwe CAS mapema kabla ya ligi kuanza ili mustakabali wake ufahamike mapema
Makundi mbalimbali ya mashabiki wa Yanga kwenye mitandao ya kijamii, wameanzisha kampeni maalum wakiitaka Kamati itoe hukumu mapema ili jambo hilo lipelekwe Mamlaka za juu
