Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amewashukuru mashabiki wa Yanga kwa mapokezi ya kihistoria waliyompa leo JNIA baada ya kutua akitokea DR Congo na wachezaji aliowasajili kutoka AS Vita Tuisila Kisinda na Mukoko Tonombe
Injinia amesema mapokezi aliyopewa ni makubwa na pengine hakutarajia
"Asanteni wana Yanga kwa mapokezi haya ya kihistoria. Ama hakika huu ni upendo mkubwa sana kwangu na kwa klabu yetu"
"SIJAPENDA KUBEBWA na sikuwa na jinsi ya kukataa kwa hali halisi niliyoikuta pale airport"
"Zaidi ya yote tuendelee kuijenga klabu yetu.... DAIMA MBELE NYUMA MWIKO"

ADVERTISE HERE