Akiyekuwa akisubiriwa kuwa kocha mkuu wa Yanga Cedric Kaze amesema kuugua kwa mkewe ndio sababu iliyomfanya ashindwe kuja nchini kujiunga na mabingwa hao wa kihistoria
Kaze amesema mkewe anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mwishoni mwa wiki hivyo aliomba kwa uongozi wa Yanga apewe muda amuuguze
"Niliwafahamisha Yanga kuhusu changamoto inayonikabili na niliwaomba wanipe muda niweze kushughulikia tatizo hilo, lakini walinifahamisha kuwa wanakabiliwa na presha kubwa kutoka kwa mashabiki hivyo wasingeweza kunisubiri, tumekubaliana na kuachana," alisema Kaze
"Nilipenda kuja kufanya kazi Yanga ila shida nimeshindwa kuigawa akili kwakuwa akili inaweza kuwa Yanga huku pia mke wangu anaumwa sana ,nimeona sitaweza kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja,na ndio maana niliwaomba Yanga wanivumilie kwa muda flan ili afya ikikaa sawa ndio nije Tanzania"
Yanga ilitangaza kuachana na Kaze jana na wakati huohuo wakimpa majukumu Juma Mwambusi wakati wakisubiri kutangaza jina la kocha mkuu