Kiungo mshambuliaji wa Yanga Farid Mussa amewataka mashabiki wa timu hiyo wajitokeze kwa wingi siku ya Jumapili wakati mabingwa hao wa kihistoria watakapocheza na Mbeya City katika mchezo wa ligi kuu ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Farid aliyetua Yanga dirisha la usajili lililopita akitokea CD Tennerife ya nchini Hispania, amesema watapambana kuhakikisha wanawapa furaha mashabiki wao baada ya kukosa ushindi kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons
"Tutahakikisha tufanya kila lililo ndani ya uwezo wetu ili kupata matokeo chanya kwenye Mchezo wetu dhidi ya Mbeya City Jumapili hii ya tarehe 13/09/202"
"Wapenzi,wanachama na Mashabiki wetu tunawaomba wajitokeze kwa wingi ili kutupa morali wa kufanya vizuri," amesema
Winga huyo ambaye pia hucheza timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), ni miongoni mwa wachezaji walioanza katika kikosi kilichotoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons
Alitoka mwanzoni mwa kipindi cha pili nafasi yake ikichukuliwa na Yacouba Sogne