Prisons wakipona leo wakatambike

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Nov 2017
Prisons wakipona leo wakatambike
Kikosi cha Yanga kinashuka leo kwenye dimba la Azam Complex, Chamazi kucheza mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 11 dhidi ya Prisons.

Yanga inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na 'afya ya kimchezo' kufuatia ushindi wake wa maao 5-0 dhidi ya Mbeya City wiki iliyopita.

Ari ya wachezaji wa kikosi cha Yanga iko juu na kuna shauku kubwa ya kuibuka na ushindi mnono kwenye mchezo huo ili kukwea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Vodacom kwani ushindi utaifanya Yanga ifikishe alama 23 hivyo kuzipiku Simba na Azam FC zenye alama 22 kila moja.

Simba itashuka dimbani kesho kuchuana na Lipuli wakati Azam FC itakuwa na kibarua kigumu keshokutwa Jumatatu itakapokabiliana na Mtibwa Sugar.

Kurejea kwa Amissi Tambwe kikosini kutaongeza hamasa ya mchezo huo. Kwa siku za karibuni Yanga imekuwa ikitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini ikitumia chache.

Akipewa nafasi, Tambwe anasifika kwa kutofanya makosa katika kutumbukiza mpira wavuni.

Mwenyewe amesisitiza leo anataka kuanza rasmi mbio za kutwaa kiatu cha dhahabu.

Walinzi wa Prisons watakuwa na kazi ya ziada ya kupambana na kasi ya mashambulizi ya kushitukiza na yasiyotabirika kutoka kila pembe ya uwanja.

Licha ya kukosekana viungo Thabani Kamusoko na Papi Tshishimbi kutokana na majeruhi, bado kikosi cha Yanga ni imara sana na kinaweza kuwaduwaza Prisons mapema tu kama ilivyokuwa kwa ndugu zao Mbeya City.

Kinara wa mabao katika kikosi cha Yanga Obrey Chirwa anahitaji mabao mawili tu kumfikia Emanuel Okwi, bila shaka kwenye mchezo huo atayasaka mabao hayo ili 'kuwanyamazisha' mashabiki wa Simba.

Ibrahim Ajib mwenye mabao matano hajafunga katika michezo mitatu iliyopita. Naye atakuwa moto wa kuotea mbali kuhakikisha anafunga ili amalize ukame wa mabao.

Hata hivyo safu ya ulinzi ya Yanga inapaswa kumchunga Mohammed Rashidi kinara wa upachikaji mabao wa Prisons.

Rashidi ana mabao sita kama ilivyo kwa Chirwa. Amekuwa akihusishwa kutaka kusajiliwa na Yanga kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.

Bila shaka atataka autumie mchezo huo 'kuishawishi' Kamati ya usajili ya Yanga impe mkataba bila kuchelewa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’