Krmpotic apongeza wachezaji kwa upambanaji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Sep 2020
Krmpotic apongeza wachezaji kwa upambanaji

Kocha Mkuu wa Yanga Zlatko Krmpotic amewapongeza wachezaji wa kikosi chake kwa kupambana kwa muda wote kuhakikisha wanaondoka na ushindi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City ambao ulipigwa jana Jumapili kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa

Bao la Lamine Moro la dakika ya 87 lililotosha kuihakikishia Yanga alama tatu muhimu

Akizungumza baada ya mchezo huo, Krmpotic alisema vijana wake walihitaji uvumilivu kuweza kumaliza mchezo huo na ushindi

"Pamoja na kuwa sikufurahishwa na namna tulivyocheza, nawapongeza wachezaji wangu walipambana kwa muda wote kuweza kupata matokeo. Haikuwa rahisi kucheza na timu ambayo imeweka wachezaji 10 nyuma ya mpira," alisema Krmpotic

"Kwa wastani sisi tulicheza mpira kwa zaidi ya asilimia 70, muda mwingi tulikuwa eneo la wapinzani wetu, ilihitaji uvumilivu na kutokata tamaa, ni ushindi tulioupigania"

"Bado tuna kazi ya kufanya kwenye timu yetu. Ukiangalia kipindi cha kwanza hatukucheza tulivyotaka, tunapaswa kuweka mpira chini lakini wakati mwingine naelewa wachezaji wangu walilazimika kutumia mipira mirefu"

Krmpotic ana siku tano za kukiandaa kikosi chake kuelekea mchezo dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa Jumamosi, Septemba 19 kwenye uwanja wa Kaitaba kule Bukoba

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’