Mauya uso kwa uso na Kagera Sugar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Sep 2020
Mauya uso kwa uso na Kagera Sugar

Keshokutwa Jumamosi mabingwa wa kihistoria Yanga watashuka uwanja wa Kaitaba kumenyana na Kagera Sugar katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom, raundi ya tatu

Huu ni mchezo utakaokuwa na sura tatu tofauti;

Kwanza ni mchezo mwanzo ambao Yanga itacheza nje ya jiji la Dar es salaam tangu kuanza kwa msimu huu

Yanga ilicheza mechi zake mbili za awali jijini Dar es salaam ikilazimishwa sare dhidi ya Tanzania Prisons na baadae kuifunga Mbeya City

Pili katika mchezo huu, kiungo Zawadi Mauya anatarajiwa kuwakabili waajiri wake wa zamani Kagera Sugar

Mauya alisajiliwa na Yanga akitokea klabu hiyo inayonolewa na Meckie Mexime

Upo uwezekano mkubwa Mauya ataanza sambamba na Mcongomani Mukoko Tonombe katika safu ya kiungo

Mauya na Mukoko walionekana kuelewana sana kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Mlandege Fc ambao ulipigwa jana uwanja wa Azam Complex na Yanga kushinda mabao 2-0

Lakini pia, huu utakuwa mchezo wa kwanza ugenini kwa kocha Krmpotic. Hiki ni kipimo chake cha kwanza juu ya mbinu ambazo anapaswa kuzitumia kwenye michezo ya ugenini

Kutakuwa na ahueni sababu uwanja wa Kaitaba ni wa nyasi bandia, anaweza kutumia falsafa yake ya kuweka mpira chini

Lakini atakapokwenda mkoani Morogoro kuifuata Mtibwa Sugar pengine atalazimika kubadili mbinu kutokana na mazingira mabovu ya uwanja wa Jamhuri

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’