Kiungo Mcongoman Mukoko Tonombe jana alifunga moja ya mabao bora kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Mlendege ambao ulimalizika kwa Yanga kushinda mabao 2-0
Mukoko alifunga bao hilo kwa shuti kali la umbali wa takribani mita 25 akimuacha mlinda lango wa Mlandege asijue la kufanya
Baada ya kufunga bao hilo, aina ya ushangili aliotumia ndio ulikuwa kivutio zaidi kwani aliwaweka wachezaji wenzake chini na kama anawaelekeza jinsi ya kufunga


Tangu ajiunge na Yanga, Mukoko ameonyesha kiwango cha hali ya juu, hakika msimu huu Wanayanga wana kila sababu ya kutembea kifua mbele kwani wana kikosi bora sana
ADVERTISE HERE