Mashabiki wamtaka Farid Mussa dimbani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Sep 2020
Mashabiki wamtaka Farid Mussa dimbani

Jina la kiungo mshambuliaji Farid Mussa limekuwa likitajwa sana na mashabiki wa Yanga kila mara anapokosekana kwenye kikosi cha kwanza

Farid bado hajajihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kocha Zlatko Krmpotic lakini mashabiki wanaamini mchezaji huyo aliyerejea nchini akitokea Hispania, anaweza kuwa na mchango mkubwa kama atapewa nafasi

Kocha wa Yanga Zlatko Krmpotic amesema winga huyo mwenye kasi bado hayuko fiti baada ya kukaa muda mrefu bila ya kucheza mpira ligi ziliposimama kutokana na janga la corona

Farid alikuwa akiitumikia klabu ya CD Tennerife inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Hispania

Alikaa nje kwa takribani miezi mitano huko Hispania wakati nchi hiyo ilipoweka lockdown mpaka pale alipofanikiwa kusafiri kujiunga na Yanga mwezi uliopita

Mashabiki wa Yanga wanatamani Krmpotic awaanzishe pamoja Farid na Tuisila Kisinda kwani kasi yao inaweza kuziletea shida timu pinzani

Mchezaji mwingine ambaye imeelezwa bado hayuko fit ni kiungo Carlinhos ambaye naye alikaa karibu miezi sita bila ya kucheza mpira

Krmpotic amempa Carlinhos dakika chache kwenye mechi mbili zilizopita lengo likiwa kumuimarisha taratibu na kumfanya aizoee ligi ya Tanzania

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’