Wikiendi hii Yanga inakwenda kutikisa pale viunga vya mkoa wa Morogoro kuelekea mchezo wake wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar ambao utapigwa keshokutwa Jumapili katika uwanja wa Jamhuri
Tayari misafara ya mabasi kutoka jijini Dar es salaam, Pwani, Dodoma na hata Singida inaelekea pale Morogoro kuongeza hamasa katika msako wa alama tatu
Afisa Mhamasishaji na Msemaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema msimu huu unapaswa kuwa wa furaha kwa kila Mwana Yanga
Amesisitiza Wananchi kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao sio Morogoro tu, kila sehemu watakapoenda kucheza

"Moja ya jambo jema kwa msimu huu ni kuhakikisha kila mwanayanga anapata furaha endelevu na ili kulihakikisha hilo linafanikiwa ni kuwaona wanayanga wakiendelea Kujitokeza kwa wingi Ili Wachezaji wapate hamasa kwenye kila Mchezo"
"Tukutane Uwanja wa Jamhuri Morogoro kwenye Mchezo wetu dhidi ya Mtibwa Sugar Jumapili hii kwa umoja na wingi wetu tuipe hamasa timu yetu. Msako wa pointi tatu muhimu," ameema Nugaz
Msimu huu Yanga imepania kutwaa ubingwa, hivyo hii ni kampeni kwa kila Mwananchi kuhakikisha anakuwa sehemu ya mafanikio ya mpango huo