Uongozi wa klabu ya Yanga umeeleza kusikitishwa na kitendo kisichokuwa cha kiungwana kilichofanywa na baadhi ya mashabiki mkoani Morogoro kwa kuwapiga mashabiki wa Simba waliofika uwanjani kushuhudia mchezo kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Yanga
Kupitia taarifa iliyotolewa na Yanga mapema leo, klabu imelaani vikali vitendo hivyo ambavyo vimeanza kujitokeza kwa wingi
"Pamoja na kusikitishwa, uongozi unalaani vikali tabia hiyo inayojengeka ya uvunjifu wa Amani katika soka na kuviomba vyombo vya ulinzi na usalama kuchunguza na hatimaye kuwachukuliwa hatua za kisheria wale wote watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo"
"Yanga tunaamini mpira ni furaha sio uadui. Tunawakumbusha mashabiki wetu kwamba upinzani wetu na SImba unatokana na utani wa jadi na sio uhasama," ilisema taarifa ya Yanga