Carlinhos atawasumbua sana mechi za mikoani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Sep 2020
Carlinhos atawasumbua sana mechi za mikoani

Juzi kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, kocha mkuu wa Yanga Zlatko Krmpotic aliwafanyia 'sapraisi' mashabiki kwa kumjumuisha kiungo fundi Carlos Fernandez 'Carlinhos' kwenye kikos chake kilichoanza mchezo huo uliopigwa uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro

Kutokana na ubovu wa sehemu ya kuchezea ya uwanja ambao tayari umefungiwa na Bodi ya Ligi, wengi hawakutarajia kumuona Carlinhos akianza

Kocha Msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi alisema ilikuwa mbinu kumuanzisha kiungo huyo na zaidi waliamua kumchezesha winga ili awe huru 'kumwaga maji'

Ni mbinu ambayo iliweza kuzaa matunda kwani ulikuwa mpira wake wa kona uliopelekea kupatikana kwa bao la Yanga lililofungwa na Lamine Moro

Kocha Krmpotic amesema ataendelea kumtumia Carlinhos katika mechi nyingine ambazo viwanja vyake ni changamoto

Mserbia huyo amesema wamekuwa wakifanya mazoezi aina ya mchezo wanaotumia katika mechi za nje ya jiji la Dar es salaam, mipira ya adhabu ni silaha muhimu kwao kutengeneza mabao Carlinhos anapokuwa uwanjani

"Ni mchezaji mwenye utaalam wa kupiga mipira. Mara nyingi krosi zake zimesababisha madhara kwenye lango la timu pinzani. Ni mchezaji tunayeweza kumtumia katika mazingira yoyote kulingana na mpango wa mechi husika," alisema Zlatko

Mpaka sasa Carlinhos amecheza mechi tatu za ligi, ametoa pasi mbili za mabao yote yakifungwa na Lamine Moro

Amekuwa akitengeneza nafasi nyingi kupitia mipira yake ya adhabu, hata hivyo bado mipira hiyo haijatendewa haki ipasavyo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’