Simba iwakemee mashabiki wake - Bumbuli

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Sep 2020
Simba iwakemee mashabiki wake - Bumbuli

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Hassan Bumbuli ameitaka klabu ya Simba iwakemee mashabiki wake kuwa wanapokwenda uwanjani kutazama mechi za Yanga waache kutumia maneno ya kejeli na kashfa kwa mashabiki wa Yanga

Aidha Bumbuli amesema hata viongozi wa timu zote wanapaswa kuacha tabia ya kuwakejeli, kuwatukana na kuwadhalilisha watu kwani mambo hayo yanaweza kuwa sababu ya chuki inayojengeka miongoni mwa mashabiki

Pamoja na kutounga mkono kitendo kilichofanywa na mashabiki wa Yanga mkoani Morogoro Bumbuli amesema ni vyema mambo haya yakaangaliwa kwa upana zaidi na kujua yanasababishwa na nini sasa kwani zamani hayakuwepo

"Simba inapaswa ikemee mashabiki wake kuwa wanapaswa kuwa wastaarabu pale wanapokwenda kutizama mechi za Yanga. Wasiingie uwanjani kwa lengo la kuwakera na kuwakejeli mashabiki wa Yanga, kejeli siku zote hazivumuliki"

"Lakini hata sisi viongozi wa hivi vilabu, tupunguze kutukana, kudhalilisha na kukera watu. Jambo hili linapandikiza chuki kwa mashabiki," alisema Bumbuli

"Unakuta shabiki wa Simba anatamba kuwa anakwenda uwanjani kuangalia mechi za Yanga kwa lengo la kuhakikisha Yanga inafungwa, hili ni jambo la hatari kwa sababu hata mtu anapokuja nyumbani kwako na kukuambia atahakikisha hulali vizuri na familia yako huwezi kumchukulia vizuri"

Jana klabu ya Yanga ililaani matukio ya vurugu viwanjani wakilitaka Jeshi la Polisi kuchukua hatua stahiki kwa wote waliohusika. TFF, Bodi ya Ligi nao walilaani matukio hayo

Ni wazi jambo hili linaweza kutatuliwa pale mashabiki watakapokuwa tayari kulinda misingi ya Amani kwa kutofanya matukio yanayoweza kuamsha hisia za watu wengine

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
34m ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
59m ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
4h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
23h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’