Watatu kuongezwa Kilimanjaro Stars

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
29 Nov 2017
Watatu kuongezwa Kilimanjaro Stars
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limempa fursa kocha Ammy Ninje kuongeza wachezaji watatu kwenye kikosi cha timu ya Bara kitakachoshiriki Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge mwaka huu.

Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao amesema kwamba wamemuambia kocha Ninje aongeze wachezaji watatu akitaka kufuatia Baraza la Vyama na Mashirikisho ya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuzipa nafasi hiyo Uganda na Rwanda.

Uganda na Rwanda zinatarajiwa kucheza fainali za ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) Januari mwakani zinazohusisha wachezaji wanaocheza Ligi za nchini mwao pekee na katika kuwawezesha kuviandaa vikosi vyao vyote, CECAFA imewapa nafasi Amavubi na The Cranes kwenda na wachezaji 23.

“Sasa baada ya kuzipa nafasi hiyo ya upendeleo Rwanda na Uganda, CECAFA pia ikasema kwa nchi nyingine zitakazoweza kuongeza wachezaji watatu kwa gharama zao wenyewe zinaruhusiwa. Nasi kwa sababu hiyo tumempa fursa hiyo mwalimu, sasa ni jukumu lake mwenyewe kuongeza au la,”amesema Kidau, kiungo wa zamani wa Milambo, Simba na Vijana ya Ilala ‘Kabakayeka’.

Kikosi cha Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ kinatarajiwa kuondoka Dar es Salaam kesho baada ya mazoezi ya siku tatu kwenda nchini Kenya, ambako michuano ya CECAFA Challenge inatarajiwa kufanyika kuanzia Desemba 3 hadi 16, mwaka huu.

Wachezaji wote walioteuliwa wapo kambini kasoro Daniel Lyanga wa Fanja ya Oman, ambaye anatarajiwa kuwasili leo.
Kikosi kinaundwa na makipa; Aishi Manula (Simba SC) na Peter Manyika (Singida United).

Mabeki ni Boniphace Maganga (Mbao FC), Gardiel Michael (Yanga SC), Kelvin Yondani (Yanga SC), Erasto Nyoni (Simba SC), Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ (Simba SC) na Kennedy Wilson (Singida United).

Viungo ni Himid Mao (Azam FC), Hamisi Abdallah (Sony Sugar- Kenya), Muzamil Yassin (Simba SC), Raphael Daudi (Yanga SC), Jonas Mkude (Simba), Shiza Kichuya (Simba SC), Ibrahim Ajib (Yanga) na Abdul Hilal (Tusker FC - Kenya).

Washambuliaji ni Elias Maguri (huru), Mbaraka Yusuph (Azam FC), Yohana Nkomola (huru) na Daniel Lyanga (Fanja FC, Oman).

Kilimanjaro Stars imepangwa Kundi A pamoja na ndugu zao, Zanzibar, wenyeji Kenya, Rwanda na waalikwa Libya, wakati Kundi B lina timu za Uganda, Zimbabwe, Burundi, Ethiopia na Sudan Kusini.

Kilimanjaro Stars itafungua dimba na Libya Desemba 3, mwaka huu mchezo ambao utafuatiwa na mechi kati ya wenyeji, Kenya dhidi ya Rwanda.

Kili Stars itarudi uwanjani Desemba 7 kumenyana na Zanzibar Heroes, Desemba 9 na Rwanda kabla ya kumaliza mechi zake za Kundi A kwa kumenyana na wenyeji, Kenya Desemba 11.

Mechi za makundi zinatarajiwa kukamilishwa Desemba 12 na Nusu Fainali zitachezwa Desemba 14 na 15, wakati Desemba 16 itachezwa mechi ya kusaka mshindi wa tatu ikifuatiwa na fainali.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
53m ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →