Kiungo Balama Mapinduzi ameanza kurejea 'mdogo mdogo' baada ya kukaa nje kwa takribani miezi mitatu kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya kifundo cha mguu
Balama ameanza mazoezi mepesi ikiwa ni dalili njema kuwa mwamba huyo anakaribia kurejea kikosini akiwa 'kamili gado'
Kurejea kwake kunamaanisha, fundi mwingine anaongezeka pale eneo la kiungo na hata winga
Katika kikosi cha Yanga Balama atakuwa kama usajili mpya kwani bado hajacheza mchezo wowote katika kikosi kilichosukwa upya msimu huu
Maana halisi ya kuwa na kikosi kipana sasa inaonekana, kwani hakuna ubishi Yanga inaweza kutengeneza vikosi viwili vyenye ushindani unaokaribiana
ADVERTISE HERE