Tunajenga kikosi cha kucheza dakika 120 - Mwambusi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Oct 2020
Tunajenga kikosi cha kucheza dakika 120 - Mwambusi

Kocha Msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amesema kwa sasa wanajenga kikosi kitakachokuwa na uwezo wa kucheza dakika 120

Pamoja na kuanza msimu kibabe, chini ya aliyekuwa kocha mkuu Zlatko Krmpotic, mabingwa hao wa kihistoria walikumbana na ukosoaji sana kwa soka walilokuwa wakicheza huku wachezaji wakionekana kutohimili mikiki ya mchezo kwa dakika zote 90

Mwambusi alikabidhiwa majukumu ya kuinoa Yanga baada ya Krmpotic kutimuliwa. Ijumaa iliyopita alipata mtihani wake wa kwanza kwa timu yake kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mwadui Fc

Mwambusi ameeleza kuridhishwa na kile aichokiona kwenye mchezo huo kutoka kwa wachezaji wake lakini muhimu zaidi amesema wanaanza program ya wiki tatu ambayo itainua fitnes ya wachezaji na kuwafanya wachezaji katika kiwango cha juu kwa mpaka dakika 120

"Tulicheza vizuri pamoja na kuwa ulikuwa ni mchezo wa kirafiki tu na tulipaswa kumpa nafasi kila mchezaji. Yapo mapungufu tuliyabaini na tunayafanyia kazi. "

"Ninataka kuona wachezaji wanakuwa na uwezo wa kucheza dakika zote 90 hadi 120 bila kuchoka, lakini kwa kiwango kile kile na spidi ile ile. Nadhani baada ya wiki tatu hivi vyote tunavyovifanyia kazi vitaanza kuonekana na kutoa matokeo mazuri zaidi," alisema Mwambusi

Katika mchezo huo ambao Yanga ilishinda bao 1-0 lililowekwa kambani na Michael Sarpong, ni Mwadui Fc waliokuwa bora zaidi kwenye kipindi cha kwanza lakini Yanga wakarejea mchezoni kwenye kipindi cha pili kiungo Carlos Carlinhos akitengeneza bao pekee kwa pasi yake ya umbali wa takribani mita 40

Baada ya mapumziko ya mwishoni mwa wiki, kikosi cha Yanga leo kinaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wa ligi kuu unaofuatia dhidi ya Polisi Tanzania ambao utapigwa Oktoba 22 uwanja wa Benjamin Mkapa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
8h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
12h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
13h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
13h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’