Kaze afunguka mwenendo wa kikosi chake

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Oct 2020
Kaze afunguka mwenendo wa kikosi chake

Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze ameeleza kufurahishwa na muitikio wa wachezaji wake katika program za mazoezi anazowapatia

Kocha huyo raia wa Burundi, ameinoa Yanga kwa takribani siku tatu sasa. Ameeleza vijana wake wanajitoa kwa moyo kuhakikisha wanafahamu kile anachowafundisha

Aidha Kaze amebainisha kuwa ni wachezaji wanne tu ambao wamekosa mazoezi kutokana na sababu mbalimbali

"Tunashukuru tumeanza vizuri, vijana wanajitoa kwa moyo mmoja, kikosi chetu kiko katika hali nzuri tunawakosa wachezaji wanne tu. Abdulaziz Makame ni majeruhi pamoja kijana Fahad aliyepandishwa kutoka timu ya vijana. Hawa wameanza program maalum za mazoezi"

"Tunafahamu majeruhi ya Mapinduzi Balama ni ya muda mrefu lakini pia tunamkosa Carlinhos ambaye ni mgonjwa," alisema Kaze

Kaze atakuwa na mtihani wake wa kwanza katika ligi kuu ya Vodacom siku ya Alhamisi, pale kikosi chake kitakaposhuka uwanja wa Uhuru kuikabili Polisi Tanzania katika mchezo utakaopigwa saa kumi Alasiri

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
11h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
15h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
20h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
23h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’