Niyonzima atuliza mzuka wa mashabiki Yanga

Admin By Admin
•
14 Jun 2017
Niyonzima atuliza mzuka wa mashabiki Yanga
Nahodha msaidizi wa Yanga Haruna Niyonzima amekuwa akitajwa na vyombo vya habari kuwa anaondoka klabuni baada ya kuitumikia Yanga kwa miaka mitano.

Sasa mwenyewe ametoa kauli kuwa hana mpango wa kuondoka jangwani na baada ya kuitumikia timu yake ya Taifa ya Rwanda, atarejea jijini Dar es salaam karibuni kusaini mkataba mpya.

“Nikwambie kitu, sidhani kama kuna mchezaji wa kimataifa kutoka nje ya nchi alidumu kuichezea klabu yake kwa muda wa miaka mitano mfululizo bila kuihama timu yake kama mimi.

“Mimi nimekaa kwa amani na kuvumilia hali zote za shida na raha, hivyo sidhani kama ni sahihi mimi kuondoka vibaya Yanga, nitaondoka lakini siyo kama inavyoelezwa.

“Bado mchezaji halali wa Yanga ninayemaliza mkataba wangu mwezi ujao, hivyo Wanayanga wasiogopeshwe na taarifa mbalimbali zinazohusiana na mimi kwenda Simba,” alisema Niyonzima.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →